Search This Blog

Tuesday, August 13, 2019

Kesi ya Lissu ya Kupinga Kuvuliwa Ubunge Kunguruma Kesho Mahakama Kuu


Kesi iliyofunguliwa na aliyekuwa mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu akipinga kuvuliwa ubunge na Spika wa Bunge, Jb Ndugai, imepangwa kuanza kusikilizwa Agosti 15, 2019 katika Mahakama Kuu ya Tanzania.

Juni 28 mwaka huu, Ndugai alilitangazia bunge kuwa ameiandikia Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) kuileleza kuwa jimbo la Singida Mashariki, lililokuwa likishikiliwa na Lissu kupitia chama kikuu cha upinzani Chadema lipo wazi.

Spika Ndugai ametaja sababu kuu mbili zilizomsukuma kuiandikia tume ya uchaguzi barua hiyo, mosi ni kutokana na Lissu kutokuhudhuria bungeni kwa muda mrefu na pili kutokuwasilisha fomu ya tamko la mali na madeni kwa sekretari ya maadili kwa mujibu wa sheria.

lissu alipinga vikali kuvuliwa ubunge kwa hoja hizo alizozitoa spika Ndugai na kudai atakwenda kufungua kesi Mahakamani kwani tangu ashambuliwe kwa risasi hadi anavuliwa ubunge bado alikuwa anaendelea na matibabu.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...