Search This Blog

Sunday, August 25, 2019

Kenya kuiuzia China maparachichi mabichi


Balozi wa Kenya nchini China Bi. Sarah Serem amesema, Kenya inafanya mazungumzo na China kuhusu kuiuzia maparachichi mabichi, baada ya kutambua makubaliano ya zamani hayawezi kuwanufaisha wakulima wadogo wa Kenya.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Beijing, China, Bi. Serem amesema nchi hizo mbili zinafanya kazi kwa pamoja ili kuhimiza biashara ya kunufaishana kati yao.

Kenya ni nchi ya pili barani Afrika baada ya Afrika Kusini kwa kilimo cha maparachichi. Maelfu ya wakulima waliopanda kahawa sasa wamegeukia kupanda miti ya maparachichi, inayojulikana kama "dhahabu ya kijani".

Kwenye mkutano wa pili wa kilele wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" uliofanyika mwezi Aprili mjini Beijing, China na Kenya zilisaini makubaliano ya kuiruhusu Kenya kuiuzia China maparachichi, ambayo yanatakiwa kuhifadhiwa katika nyuzijoto 30 chini ya sifuri baada ya kutolewa ngozi, na kusafirishwa katika chombo chenye nyuzijoto 18 chini ya sifuri. Hali hii itawalazimu wakulima wa Kenya kujenga vyumba vya baridi na kununua zana husika. Lakini asilimia 70 ya wakulima wanaopanda maparachichi hawana uwezo huu.

Bi. Serem amesema, wataalam wa China wamefanya ziara ya pili mwezi Julai nchini Kenya baada ya kuitembelea mwezi Machi, ili kufanya tathmini. Sasa suala wanaofuatilia zaidi ni nzi wa kwenye matunda wanaoweza kuhamia China kutokana na maagizo ya maparachichi mabichi. Hata hivyo ametarajia kuwa pande hizo mbili zitafikia makubaliano haraka.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...