Nahodha wa Klabu ya KMC Juma Kaseja amesema kwasasa amepona, jereha la kichwa alilopata kwenye mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya CHAN dhidi ya Kenya.
Akiongea leo kwenye makao makuu ya KMC, Kaseja amesema yeye yupo vizuri kuipigania timu yake hiyo kwenye mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya AS Kigali siku ya Ijumaa.
''Nimetibiwa vizuri na daktari amesema nimepona hivyo niko sawa, watanzania waungane kwa pamoja kwasababu timu inawakilisha taifa, sisi tutakuwa uwanjani kuhakikisha tunatimiza hitaji la kila mtanzania ambalo ni kufuzu hatua inayofuata'', ameeleza.
KMC itakuwa kwenye uwanja wa taifa Ijumaa Agosti 23, 2019 kucheza mchezo wa marejeano na AS Kigali. Mchezo wa kwanza huko Kigali ulimalizika kwa suluhu, hivyo KMC wanahitaji ushindi wowote ili kusonga mbele.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment