Search This Blog
Monday, August 5, 2019
Hospitali ya Taifa Muhimbili yakanushwa kuwa na Mgonjwa Mchawi
Hospitali ya Taifa Muhimbili imekanusha taarifa zinazosambaa katika mitandao ya kijamii, moja ikiwa ni video na nyingine ni sauti ikieleza kuhusu video hiyo kuwa ni mama mchawi amelazwa ‘Hospitali ya Muhimbili’
Imesema video hiyo sio hospitali ya Muhimbili kwa sababu, kwanza hakuna mgonjwa huyo wala hakuna wodi inayofanana hivyo katika hospitali hizo (Upanga na Mloganzila) na sare zilizovaliwa na wauguzi sio za hospitali hizo
Aidha, imebainisha kuwa wanafanyia kazi taarifa hiyo kwa ushirikiano na mamlaka husika ili kibaini aliyesambaza taarifa hiyo ya upotoshaji na udhalilishaji kwa mgonjwa yule na hatua stahiki zitachukuliwa akibainika
Video inayosambaa inamuonesha mwanamke huyo akiwa amezungukwa na Wagonjwa, Waangalizi wa wagonjwa na Wauguzi kwenye wodi ya hospitali akikemewa na kutakiwa aondoke baada ya kudaiwa kuwa anajigeuza kuwa ndege usiku na kuwa binadamu asubuhi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment