Search This Blog
Saturday, July 6, 2019
Waziri Hasunga afanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Mbolea ya nchini Misri
Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga amekutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya TOPIC ya Mjini Cairo nchini Misri Mhandisi Raouf Bakry katika kikao kazi kilichofanyika Ofisi za Wizara ya Kilimo Jijini Dar es salaam.
Katika mkutano huo Mhandisi Raouf amemueleza Hasunga kuwa lengo la ziara yake ni kuangalia uwezekano wa kutumia fursa inayopatikana na kutolewa na Benki ya EXIM inayotoa mikopo nafuu ili kufanya biashara kati ya nchi za Afrika.
Amesema kuwa akipatiwa mkopo huo ataongeza uwezekano wa kusambaza mbolea na viuatilifu ili kuongeza tija na kasi ya uzalishaji wa mazao mbalimbali ya wakulima.
Kwa upande wake, Waziri wa Kilimo,Japhet Hasunga amemueleza Mhandisi Raouf kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli imedhamiria kutekeleza kwa vitendo hivyo ina wakaribisha wawekezaji katika uwekezaji mbalimbali ikiwemo sekta ya viwanda vya kusindika mazao.
Alisema kuwa Mhe Magufuli amejipambanua katika kuimarisha uwezekano wa wawekezaji kuwa na uwekezaji uliotukuka ili kuwanufaisha watanzania sambamba na manufaa kwao wenyewe.
Katika mkutano huo baina ya Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya TOPIC ya Mjini Cairo nchini Misri Mhandisi Raouf Bakry ulihudhuriwa pia na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya mbolea ya Taifa (TFC) Ndg Salum Mkumba.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment