Search This Blog
Saturday, July 27, 2019
Wasukumwa Jela Miaka 20 kwa Kukutwa na Nyama ya Pundamilia
Mahakama ya Hakimu mkazi mfawidhi wilaya ya Serengeti Mkoani Mara, leo Julai 26, 2019, imewahukumu miaka 20 jela kila mmoja washtakiwa wanne kwa kosa la uhujumu uchumi.
Kesi hiyo namba 55 ya mwaka 2018, imetolewa hukumu na Hakimu Ismael Ngaile, ambapo inaelezwa washtakiwa hao walikamatwa mwaka 2018, katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na kukutwa na nyama ya Pundamilia pamoja na miguu ya mnyama huyo.
Watuhumiwa hao James Mwita na Yohana Mahende, wakazi wa Kisangura walikutwa na nyama hiyo yenye thamani ya shilingi 2,616,000, huku wenzao Athuman Zakaria na Juma Chacha walikutwa na miguu ya mnyama huyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment