Search This Blog
Sunday, July 7, 2019
Wafa maji wakikwepa kushambuliwa na Viboko Ziwa Babati
Na John Walter, Babati
Watu wawili wamepoteza maisha wakati wakiwa kwenye shughuli zao za uvuvi wa samaki Ziwa Babati mkoani Manyara usiku wa kuamkia jana.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Manyara Augustino Senga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa miili ya watu hao Paulo Elias(45) na Nicomed Peter (43) wote wakazi wa mtaa wa Nangara mjini Babati,walikutwa wakiwa pembezoni mwa ziwa hilo huku mitumbwi waliyokuwa wakiitumia ikielea juu ya maji.
Kamanda Senga ameeleza kwamba miili hiyo ipo hospitali ya mji wa Babati Mrara kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Ziwa hilo linakisiwa kuwa na viboko wengi ambao wanahatarisha maisha ya wakazi wanaozunguka ziwa hilo pamoja na wavuvi kwani ndani ya siku mbili pekee tayari watu watatu wamepoteza maisha wakijihami na Viboko hao
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment