Search This Blog
Sunday, July 7, 2019
Rais Mstaafu Jakaya Kikwete asifu Maonesho ya 43 ya Sabasaba
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete amezipongeza Wizara ya Viwanda na Biashara na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) kwa maandalizi mazuri ya Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere.
Akizungumza Jumamosi hii mara baada ya kutembelea na kukagua mabanda mbalimbali ya washiriki wa Maonesho hayo, Rais Mstaafu Kikwete alisema hizo ni dalili njema kwa maonesho hayo kwa kuwa yamekuwa bora zaidi ya maonesho yaliyofanyika mwaka jana.
Aidha aliongeza kuwa maonesho ya mwaka huu, yameonesha dhamira ya dhati ya Serikali katika kujenga uchumi wake kupitia viwanda, kwa kuwa katika maonesho ya mwaka huu malighafi nyingi za kilimo zimepewa kipaumbele na wazalishaji wa bidhaa mbalimbali.
“Maonesho ya mwaka huu yamekuwa bora zaidi, kwani tumeshuhudia malighafi nyingi za kilimo zikipewa kipaumbele na hii imekuwa ni dalili njema na point (alama) tunayotakiwa kuifikia kwa sasa” alisema Kikwete.
Awali akitembelea Banda la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Rais Mstafu Kikwete alilitaka jeshi hilo kuwa wabunifu kwa kuzalisha bidhaa bora zitakazoweza kutumika nje ya Tanzania hususani bidhaa za ngozi ikiwemo viatu vinavyozalishwa na Jeshi hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment