Search This Blog
Saturday, July 20, 2019
Nimemnunulia Wema Kiwanja, ila Tunapeana Lawama- Martin Kadinda
Mbunifu wa mavazi hapa nchini Tanzania Martin Kadinda, ameeleza mengi ikiwemo kumnunulia kiwanja staa na muigizaji Wema Sepetu, na kile kinachoendelea kwa sasa kati yake ana Wema pamoja na Petitman Wakuache.
Martin Kadinda amefunguka hayo kupitia EATV & EA Radio Digital, baada ya kuulizwa kuhusu suala la ndoa na ujenzi kwa mtu wake wa karibu ambaye ni Wema Sepetu.
"Ni mtu wangu na ni familia yangu tumekaa kwa miaka 10, namshauri vitu vingi vingine anavifanya vingine anarudia, siwezi kumshauri aolewe yule ni mwanamke anatakiwa kufanya maamuzi mwenyewe, mimi nilimkabidhi Wema kiwanja kwenye sherehe ya kuzaliwa kwake mwaka 2015, kama amejenga au hajajenga hayo ni mambo yake binafsi".
Aidha mbunifu huyo wa mavazi amesema kwa sasa ukaribu wake na Wema Sepetu pamoja na Petitman Wakuache, wameamua kuutoa kwenye vyombo vya habari kwa sababu mara nyingi wanabebeana lawama, anaweza akafanya jambo Wema akalaumiwa yeye, au akafanya Martin Kadinda akalaumiwa Wema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment