Search This Blog
Saturday, July 13, 2019
Mtoto Wa Makonda Katimiza Mwaka Mmoja Huu ndo Unumbe Alomtumia
Kupitia ukurasa wa instagram, Paul Makonda ambaye ni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ameandika ujumbe kwa kina mama wanaohangaika kupata mtoto, walioteseka na kudharaulika na hadi wengine kufikia hatua ya kuitwa mpaka tasa
Ninapokumbuka siku kama ya leo Kwa mwaka uliopita nayaona machozi Mengi ya furaha kwangu kwa mke wangu na ndg zangu juu ya Muujiza huu Mkubwa ktk maisha yetu.
Kwa sababu hii naomba niseme jambo moja kwa Wakina mama wengi sana ambao wamebakia na vidonda vya kudumu moyoni baada ya morning kuchukiwa,kusingiziwa vya uongo na kutuhumiwa na ndugu au waume zao kwa kukosa watoto.Wengi tunasahau kuwa mtoto ni zawadi anayotupa Mungu.
Wapo ambao hadi wameachwa huku wakinenewa maneno magumu ya kuvunja moyo.Leo ningependa niwape pole wote mliopitia nyakati hizi katika maisha yenu.
Jambo kubwa ambalo ningependa kukumbusha ni kuwa pamoja na juhudi za kibinadamu za kidaktari,pamoja na maombi ya kila aina tunayoweza kufanya mbele za Mungu,pamoja na mipango mingi kuhusu kupata mtoto:JIBU LA MWISHO HUTOKA KWA MUNGU.
Mama yangu unayepitia changamoto hii endelea kumtumaini Mungu ATAFANYA KWA WAKATI WAKE kwani yeye HAWAHI wala HACHELEWI.
Nakuombea kwa Mungu,Usife Moyo.Ipo siku utaitwa mama ewe ulieitwa Tasa Kwa jina la Yesu mwana wa Mungu aliye hai.
Amen
Ni Mimi Paul Makonda ndg yako katika Kristo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment