Search This Blog

Tuesday, July 30, 2019

Mchungaji Maarufu duniani athibitisha kuvunjika kwa ndoa yake


Aliyekuwa mchungaji, Joshua Harris amethibitisha kuvunjika kwa ndoa yake, pia ameiomba msamaha jamii ya LGBTQ na kusema yeye si mkristo tena.

Joshua alijizolea umaarufu kupitia kitabu chake (I Kissed Dating Goodbye) kilichopinga kujamiiana kabla ya ndoa na mapenzi ya jinsia moja.

Katika kitabu hicho kilichotoka mwaka 1997, Joshua ambaye ni mwandishi kutoka Marekani alipinga mahusiano ya jinsia moja, huku akiwaasa vijana kutojamiiana hadi watakapofunga ndoa kwani hicho ndicho kinachompendeza Mungu.

Lakini kwa sasa ameomba msamaha kwa kile alichoeleza kwamba mafundisho katika kitabu hicho yaliwatenga baadhi ya watu (LGBTQ) na kutotambua nafasi yao katika jamii, pamoja na kupingana na wale waliokuwa na mtazamo tofauti naye.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...