Search This Blog

Saturday, July 6, 2019

Mbwana Samatta awakumbuka viongozi wa Simba SC na TFF


Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta amebainisha kuwa amejaribu kuwatembelea gerezani viongozi wa zamani wa klabu ya Simba ambao ni makamu wa Rais Godfrey nyange 'kaburu'  na Rais wa TFF, Jamali Malinzi lakini hakufanikiwa kuwaona.

Samatta ambaye alikuwa na Taifa Stars nchini Misri ilikokuwa ikishiriki AFCON 2019 na kutolewa hatua ya makundi amesema licha ya kutowaona lakini anawaombea.

Kikosi cha Taifa Stars kilirejea kutoka nchini Misri ambapo kilicheza mechi tatu za Kundi C dhidi ya Senegal, Kenya na Algeria lakini kikapoteza mechi zote.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...