Search This Blog

Sunday, July 28, 2019

Maskini..Miili 25 ya Watoto Wachanga Yapatikana Kwenye Makaburi Ivory Coast


Miili 25 ya watoto imelipatikana kwenye makaburi kaskazini magharibi mwa Ivory Coast.

Vyombo vya habari vimeripoti kwamba polisi wamepata miili ya watoto 25 kwenye makaburi katika mji wa Gagnoa, kilomita 230 kutoka mji mkubwa zaidi nchini, Abidjan.

Maafisa wa polisi, wamesema miili hiyo imepatikana baada  ya polisi kuona vifaa vya  kuchimbia katika makaburi hayo.Walipofanya utafiti wakakutana na begi jeusi lililojaa miili 25 ya  watoto iliyooza.

Mamlaka imeanzisha rasmi uchunguzi wa tukio hilo kwani huenda ukawa na uhusiano na mila za kishirikina.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...