Serikali ya Marekani imeidhinisha adhabu ya kifo ianze tena kutekelezwa, baada ya adhabu hiyo kusitishwa miaka 16 iliyopita, ambapo imehalalishwa kisheria katika majimbo 29 nchini humo.
Katika taarifa iliyotolewa na mwanasheria mkuu wa nchi hiyo, William Barr amesema kuwa tayari ameiagiza Halmashauri ya Magereza, kupanga siku ya kunyongwa kwa wafungwa watano waliopewa adhabu hiyo, ambao walishtakiwa kwa kuhusika na mauaji na ubakaji wa watoto na watu wazima na hukumu yao imepangwa kutekelezwa Disemba 2019 na Januari 2020.
Aidha, mwanasheria huyo ameiagiza Halmashauri ya Magereza, kubuni sera itakayoidhinisha matumizi ya dawa moja kwaajili ya kumuua mtu, badala ya kutumia aina tatu za dawa ambayo ilikuwa ikitumika hapo mwanzo
Adhabu ya kifo ilitekelezwa mara ya mwisho mwaka 2003 dhidi ya Louis Jones Jr (53), mbabe wa vita vya Ghuba aliyemuua askari wa miaka 19 Tracie Joy McBride.
Kwa mujibu wa taarifa zilizokusanywa na kituo kinachonakili taarifa kuhusu adhabu ya kifo, watu 78 walihukumiwa adhabu ya kifo kati ya mwaka 1988 na 2018, lakini ni watu watatu tu kati ya hao waliouawa.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment