Search This Blog
Saturday, July 6, 2019
Jeshi la Polisi lawanasa raia 3 wa kigeni wakisafirisha Madini
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu watatu raia wa kigeni kwa kosa la kusafirisha madini aina ya dhahabu bila kuwa na kibali.
Watuhumiwa hao walikuwa wakitokea Wilaya ya Chunya kuelekea Jijini Dar es salaam.Watuhumiwa hao ni 1: Clive Rooney (62)raia wa nchi ya Ireland 2: Ross Stephen Chertsey (34), raia wa nchini Uingereza pamoja na 3:Robert Charles 58, raia wa nchini Uingereza.
Tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 03.07. 2019 huko Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Songwe (SIA), Kata ya Nsalala,Tarafa ya Usongwe Wilaya ya Kipolisi Mbalizi. Watuhumiwa hao walikamatwa na maafisa wa usalama wa uwanja huo wa Songwe.
Madini hayo yalikuwa na uzito wa gramu 1,044.95. Ufuatiliaji unaendelea kufanywa na Kikosi kazi cha kamati ya usalama ya Mkoa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment