Search This Blog
Tuesday, July 30, 2019
Aliyemuua mke wake na kumteketeza kwa magunia ya mkaa asomewa shtaka la mauaji
Mfanyabiashara Khamis Luwongo maarufu kwa jina la Meshack (38), anayedaiwa kumuua mke wake kwa kumchoma na magunia mawwili ya mkaa amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam na kusomewa shtaka la mauaji.
Akisoma hati ya mashtaka leo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Saimon mbele ya Hakimu Mkazi, Salum Ally alidai kuwa mshtakiwa anatuhumiwa kwa kosa moja la mauaji Kinyume cha Sheria ya kanuni ya adhabu namba 196 sura 16 kama kikivyofanyiwa marejeo 2012.
Wankyo alidai kuwa mshtakiwa huyo ambaye ni Mkazi wa Kigamboni, Dar es Salaam anatuhumiwa Mei 15, 2019 akiwa Gezaulole eneo la Kigamboni alimuua mtu anayeitwa Naomi Marijani .
Baada ya kumaliza kusoma shtaka hilo, Wankyo alidai kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika, hivyo naomba tarehe ya kutajwa.
Hakimu aliahirisha Kesi hiyo hadi Agosti 13, mwaka huu kwa kutajwa na kuangalia kama upelelezi umekamilika au la.
Kabla mshtakiwa kusomewa shtaka lake, Hakimu Ally alimtaarifu kuwa Mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo, atasomewa shtaka lake, atasikiliza ila asijibu chochote.
Wakati mshtakiwa huyo anatolewa mahabusu na kupandishwa mahakamani, alifunika sura yake kwa kutumia kofia ya koti lake kwa lengo la kutokuonekana sura yake.
Mshtakiwa huyo anatuhumiwa kumuua mkewe Naomi Marijani (36), Mei mwaka huu katika maeneo ya Kigamboni jijini Dar es Salaam na kisha kuripoti polisi mkewe huyo ametoweka nyumbani na kwamba amemtumia ujumbe kuwa amemuachia mtoto wake amlee vizuri kwani amechoka na mambo yake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment