Search This Blog

Friday, June 28, 2019

Yanga Yajipanga Kusaini Kifaa Kingine AFCON

JINA la mshambuliaji Rashid Mandawa lipo kwenye orodha ya mastaa wanaotakiwa pale Yanga.



Kama ulikuwa unajua kuwa Yanga wamemaliza kufanya usajlli wa washambuliaji basi umejidanganya kwani wapo kwenye mpango wa kumsainisha Mandawa ambaye yupo kwenye michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) inayoendelea
nchini Misri.



Mshambuliaji huyo ambaye anaitumikia BDF XI ya Botswana, inadaiwa yuko kwenye mipango ya Kocha Mwinyi Zahera hivyo ni kati ya mastaa wazawa ambao wanatakiwa Yanga.



“Mandawa yupo kwenye ile orodha ya mwalimu ambapo alisema kuwa tumsainishe kwa kuwa ni mzawa kwani anaweza kutuongezea kitu. Hata hivyo hajatubana zaidi alisema tumsajili kama fedha itapatikana,” kilisema chanzo.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...