Search This Blog
Wednesday, June 5, 2019
Waziri Mkuu awataka Waislamu wote kuitumia siku ya Eid kutenda mema
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka waislamu wote nchini watumie siku kuu ya Eid el Fitr kwa kutenda matendo mema pamoja na kuwakumbuka yatima na wajane.
“Leo ni siku kubwa na muhimu waislamu wanahitimisha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kusherehekea siku kuu ya Eid El Fitr, hivyo tuendeleze matendo mema.”
Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati aliposhiriki swala ya Eid El Fitr katika msikiti wa Anwar uliopo Msasani jinini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu amesema wakati huu ni mzuri kwa kuimarisha mshikamano miongoni mwenu na madhehebu mengine, hivyo hakikisheni mnayaendeleza mambo mema yote.
“Tumeona utulivu uliojitokeza katika mwezi mtukufu, na jambo hili limesisitizwa na viongozi wa dini. Tuendelee kuwa wamoja, tuimarishe mshikamano na tuvumiliane.”
Pia, Waziri Mkuu amewakumbusha wazazi na walezi kuwaongoza watoto kwa kuwapa mafundisho ya dini yatakayowawezesha kumjua Mwenyezi Mungu na kuwa raia wema.
Awali, Imamu wa msikiti huo, Sheikh Mhina alisema waislamu wanatakiwa kuitumia siku ya leo kwa kuhamasisha Amani pamoja na kuwasaidia watu wasiokuwa na uwezo.
Pia amewasisitiza wayaendeleze mema yote waliyoyafanya katika kipindi cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani ikiwa ni pamoja na kuwaheshimu na kuwajali wazazi wao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment