Watu 17 wamepoteza maisha na watu tisa hawajulikani walipo baada ya mvua kubwa kupiga eneo la kusini magharibi mwa China la Guangxi Zhuang, idara ya usimamizi wa dharura ya kikanda ilitangaza Jumatano.
Zaidi ya watu 590,000 wameathiriwa na mvua hiyo tangu mwanzo wa wiki, kulingana na tarifa ya hivi karibuni siku ya Jumatano.
Watu zaidi ya 30,000 wamehamishwa kutoka makazi yao. Mafuriko yaliyotokea kutokana na hiyo mvua kubwa imeharibu zaidi ya hekta 34,600 za mazao. Jumla ya nyumba 1,747 zimeaanguka na 966 ziliharibiwa sana.



No comments:
Post a Comment