Search This Blog

Saturday, June 15, 2019

Watatu Mbaroni Kwa Kuhusika na Mauaji ya Katibu wa Chadema



Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya katibu mwenezi wa CHADEMA Wilaya ya Malinyi, Lucas Lihambalimu (42)

Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Wilbroad Mutafugwa amesema tukio hilo la mauaji lilitokea Juni 13 saa 8 usiku na uchunguzi uliofanywa umebainika chanzo cha mauaji ni  mgogoro wa mashamba

Kufuatia shambulio hilo, Askari walifika eneo la tukio na kukuta kipande kidogo cha chuma chenye umbo la duara kinachotumika katika bunduki zilizotengenezwa kienyeji

Aidha, mwili wa katibu huyo, ulifanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya mazishi  - #regrann  



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...