Search This Blog

Tuesday, June 11, 2019

Wagunduzi wa Madini wakingiwa kifua


Kamishna wa Madini,  Prof. Abdulkarim Mruma, amezitaka serikali za mitaa hususani ofisi za wakuu wa wilaya kuwarasimisha maeneo wananchi wanaogundua madini katika mfumo usio rasmi mara baada ya wananchi hao wanapogundua madini kwa kuokota kwenye maeneo mbalimbali ili kuepusha migogoro ambayo imekuwa ikijitokeza mara baada ya wananchi hususani wachimbaji wadogo na kisha kuvamiwa na wachimbaji na wawekezaji wakubwa

Prof. Mruma amesema hayo wakati wa mazungumzo baina ya Tume ya Madini chini ya Mwenyekiti wake Prof. Idris Kikula na Mkuu wa Wilaya (DC) ya Nachingwea Rukia Muwango walipo mtembelea ofisini  kwake kwa mazungumzo, na hiyo ni mara baada ya kumalizia kikao cha awali kilicho ikutanisha baina ya viongozi wa juu wa tume ya madini na wafanyakazi wa tume hiyo mkoa wa Lindi kwenye ofisi zao zilizopo wilayani Nachingwea jana.

Prof. Mruma amesema serikali za mitaa zinawajibu wa kulinda haki ya wananchi wanaogundua madini kwenye maeneo mbalimbali nchi ili kuwapa umiliki kwa kuwatambua wenyewe binafsi na eneo ambalo madini hayo huokotwa kabla ya kwenda kwenye ofisi za maafisa madini wa kazi waliopo nchi nzima.

Amesema na kuongeza kuwa wananchi nao wanapogundua madini au kuokota katika maeneo yasiyo rasmi hatua ya kwanza wakimbilie kwenye ofisi za serikali za mitaa kwenda kuripoti na ofisi hizo mara moja ziwatambue watu hao na mahali walipogundulia ili wasiporwe na wajanja.

“Naziomba serikali za mitaa hususani ofisi za wakuu wa wilaya ziwarasmishe kwa kuwatambua wao wenyewe na eneo husika walilogundua madini hayo ili kuleta udhibiti wa eneo kwa kuwatambua wahusika mapema kabla ya mgogoro ya umiliki.

Amesema mara nyingi inapotokea hali kama hiyo kumekuwa na uwezekano wa wananchi kuporwa haki ya umiliki wakati mwingine na vyombo vya serikali bila wao kujiju hasa inapogundulika kuwa na madini wenye nguvu hukimbia mara moja kukata leseni ya eneo hilo na kuanza kuwafukuza waliogundua au wakati mwingine hata kuandikwa leseni jina la mtu asiyejulikana ili apewe mwekezaji mkubwa.” amesema Prof. Mruma.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya amemshukuru prof. Mruma kwa kumpa elimu hiyo ambayo amesema ni muhimu kwani kwa kufanya hivyo inalinda haki ya mtu. Amesema hata Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania anathimini wagunduzi wa madini ndio maana alitoa Milioni 100 kwa mgunduzi wa Tanzanite hivyo sisi pia tunao  wajibu wa kuwalinda kwa kuwarasmisha kwa kuwatambua wagunduzi hao ili maeneo hayo yasivamiwe na wajanja.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...