Search This Blog

Wednesday, June 5, 2019

Wafanyabiashara wa mazao ya Misitu waishukuru Serikali kwa hili


Na. Amiri kilagalila, Njombe

Kufuatia Serikali  kuruhusu mazao ya Misitu ya kupandwa kusafirishwa masaa 24 baadhi ya wafanyabiashara wa mazao hayo hususani zao la mbao mkoani Njombe wameipongeza Serikali kwa hatu hiyo ambayo inalengo la kuchochea biashara ya Mazao hayo.

Wakizungumza na Muungwana blog katika soko la mbao la kambarage mjini Njombe wafanyabiashara wa mazao ya misitu Wamesema kuwa wanatumia muda mfupi kufikisha mazao sokoni na kutengeneza faida kubwa tofauti na ilivyokuwa awali waliporuhusiwa kusafirisha mazao hayo kwa masaa 12 tu.

''Kwasasa biashara imekuwa nzuri kwasababu unapiga tripu nyingi tofauti na mwanzoni,saivi unawahi na hata sisi wenyewe tunapata hela,kwanza mwanzoni ulikuwa ukitoka Njombe na ukalala Morogoro au Ruaha lakini kwa sasa ni moja kwa moja mpaka dar es salaam hakika biashara imekuwa rahisi''alisema Gideoni haule mfanyabiashara na Adrea kibasa Dereva

Licha ya kuishukuru serikali kwa hatua hiyo baadhi ya wafanyakazi katika soko hilo wameiomba serikali kuongeza ulinzi katika vituo vya ukaguzi majira ya usiku ili kuepuka baadhi ya wafanyabiashara wasio kuwa waaaminifu kusafirisha bidhaa za magendo nyakati za usiku.

''Mimi niishauri serikali sasa kuongeza ulinzi usiku kwasababu kama yalizuiwa kutembea usiku kwa kuhofia kusafirisha mali tofauti na halali hili kwasasa linaweza kuongezeka,maana wengine watatumia mwanya huo,'' alisema Brown Ngimbuchi mfanyakazi ndani ya soko la mbao Njombe.

Kuanzia mwezi mei 24 mwaka huu serikali kupitia tangazo katika gazeti la serikali namba.417 [GN417] imetoa ruksa mazao ya misitu kusafirishwa kwa masaa 24.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...