Search This Blog
Monday, June 24, 2019
Vita ya NICKI Minaj na Miley Cyrus Yafika Pabaya
Baada ya bifu la Nicki Minaj na Cardi B kupoa kwa muda sasa Nicki amehamishia majeshi kwa Miley Cyrus kwa kosa la kumchana Minaj kupitia wimbo wake wa hivi karibuni, Cattitude.
Rapa Nicki minaj ameamua kufunguka na kumtolea uvivu Miley Cyrus kupitia ‘episodi’ mpya ya kipindi chake cha Queen Radio ambapo Nicki ametoa siri za Miley kutembea na watayarishaji wa muziki ili wamtoe kimuziki na ameweka wazi mahusiano ya mtayarishaji wa muziki Mike Will na Miley Cyrus.
Aidha Nicki Minaj amesema kuwa imekuwa ni tabia ya Miley kutembea na baadhi ya watayarishaji wa muziki ili abaki kwenye chati na kujulikana zaidi.
Miley Cyrus alimchana rapa Nicki kwenye wimbo wa Cattitude ambapo aliimba “Ilove Nicki but I listen to cardi” yaani nampenda Nicki lakini namsikiliza Cardi.
Hatahivyo bifu la wawili hawa lilianza mwaka 2015 ambapo Miley alimkosoa Nicki Minaj kupitia New York Times baada ya kulalamika kunyimwa tuzo ya video bora ya mwaka Anconda kwenye MTV Awards.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment