Search This Blog

Tuesday, June 18, 2019

Serikali yampa tano Mwinyi Zahera


Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa aliipongeza Yanga kwa kuwa licha ya kucheza ligi msimu uliomalizika lakini walipambana vikali na kushika nafasi ya pili na kwamba hawakubebwa.

“Yanga ilikuwa na hali mbaya, lakini ilipambana yenyewe na kushika nafasi ya pili niwapongeze sana na niseme Yanga haikubebwa ilipambana,” alisema Majaliwa kwenye Kubwa Kuliko ya Yanga.

Aidha Majaliwa alimpongeza Kocha Mwinyi Zahera akisema kocha huyo ni kocha mzuri ambaye alioisaidia klabu hiyo.

“Mimi kitaaluma ni kocha pia ni mkufunzi niseme Zahera ni kocha mzuri aliyeisaidia sana Yanga, mwisho niseme hakuna Ligi bora bila Yanga imara na hakuna simba imara bila Yanga imara.”

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...