Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imesema maelekezo yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi kuhusu makundi yanayotakiwa kupewa vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo si ya serikali. Wizara hiyo imewataka viongozi kuzingatia maelekezo yaliyotolewa juu ya ugawaji wa vitambulisho hivyo.
Kauli hiyo imetolewa jana bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Mwita Waitara baada ya wabunge kupitisha bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi 2019/2020.
"Tamko linaloendelea kwenye mitandao likimuhusisha Mkuu wa mkoa Iringa sio maelekezo ya Serikali, ninatoa wito kwa Wakuu wote wa mikoa kuzingatia maelekezo yaliyotolewa na Serikali kuhusu vitambulisho vya Wajasiriamali” alisema.
“Hivyo ninatoa wito kwa wakuu wote wa mikoa, watendaji wote kuzingatia maelekezo yaliyotolewa na serikali kuhusu ugawaji wa vitambulisho vya wafanyabiashara na watoa huduma wadogo,” alisisitiza.
Amesema lengo la Serikali ni kuwatambua wafanyabiashara wadogo na watoa huduma wadogo ambao mauzo ghafi yao hayazidi Tsh. Milioni 4 kwa mwaka. Pia awe anatambulika kama mfanyabiashara ama mtoa huduma mdogo kupitia ofisi ya mtendaji wa mtaa ama kijiji kwa mujibu wa sheria.
Amesema hadi kufikia Mei 26, jumla ya vitambulisho milioni 1.85 vimegawiwa kwa wakuu wote wa mikoa Tanzania Bara. vitambulisho 1,176,305 vimegawiwa kwa wafanyabiashara na watoa huduma wadogo na tayari Tsh. Bilioni 23.5.

No comments:
Post a Comment