Search This Blog

Monday, June 3, 2019

Serikali kuwajengea watumishi nyumba bora


Serikali itaendelea kuwajali watumishi wa umma nchini kwa kuwajengea nyumba bora za gharama nafuu.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk Mary Mwanjelwa.

Alisema hayo alipotembelea miradi ya ujenzi wa nyumba za watumishi wa umma Gezaulole, Kigamboni na Bunju B, Dar es Salaam. Miradi hiyo ni sehemu ya ujenzi wa nyumba inayotekelezwa na Watumishi Housing Company katika maeneo mbalimbali nchini.

Dk Mwanjelwa alisema baada ya ziara hiyo ameridhika nyumba zilivyojengwa kisasa na za gharama nafuu kwa ajili ya makazi ya watumishi wa umma na wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii ambao ndio walengwa wake.

Aliwaagiza watendaji wa Watumishi Housing Company kuhakikisha wana mkakati wa kutoa taarifa kwa watumishi wa umma juu ya uwepo wa nyumba walizojenga, sehemu zilipo na bei elekezi kwa wanaohitaji kununua au kupanga.

Dk Mwanjelwa amekamilisha ziara yake ya kikazi mkoani Dar es Salaam ya kukagua miradi ya ujenzi wa nyumba za makazi ya Watumishi wa Umma na wanachama wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na kuhimiza uwajibikaji kwa watendaji wa Watumishi Housing Company.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...