Search This Blog
Sunday, June 23, 2019
Gavana Mzava asisitiza ulinzi shirikishi Ilemela
Na James Timber, Mwanza
Gavana wa Wilaya ya Ilemela Ndugu Godfrey Mzava amewasisitiza wananchi wa wilaya hiyo juu ya umuhimu wa kuwa na ulinzi shirikishi utakaosaidia kupambana na kupunguza vitendo vya kiharifu hasa vile vya ukabaji na unyang’anyi.
Rai hiyo ameitoa wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Kiseke ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kuhamasisha utekelezaji wa shughuli za maendeleo hasa ujenzi wa madarasa na miundombinu ya afya, kutoa elimu juu ya katazo la matumizi, usambazaji na uzalishaji wa mifuko ya plastiki ambapo amewataka wananchi hao kuhakikisha wanakuwa na vikundi vya ulinzi shiriki ili kupambana na vitendo vya kiharifu vinavyoendelea katika kata hiyo baada ya kutokea matukio kadhaa ya ukabaji na uporaji mida ya usiku
"Niwaombe kuhakikisha tunaanzisha vikundi vya ulinzi shirikishi ili kupambana na vitendo hivi vya kiharifu vinavyoendelea ndani ya kata yetu, Na hawa waharifuhawatoki mbali tuko nao kila siku katika maeneo yetu tuungane pamoja na vyombo vya usalama kuwadhibiti," alisema.
Aidha Gavana Mzava ametumia mkutano huo na wananchi kuendesha zoezi la upigaji wa kura za Siri ili kuwafichua watu wanaodhaniwa kuwa ni waovu wanaotekeleza vitendo hivyo vya kiharifu na baadae kumkabidhi polisi wa kata ya Kiseke maajina hayo kwaajili ya upelelezi zaidi huku akiwahakikishia wananchi hao kuwa yeyote atakaebainika kuhusika na matukio hayo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Kwa upande wake afisa mtendaji wa kata ya Kiseke, Kwa niaba ya wananchi wa kata hiyo, Amemshukuru Gavana Mzava kwa ziara yake yenye tija kwa wananchi anaowahudumia huku akibainisha shughuli za maendeleo zinazoendelea ndani ya kata yake, Pamoja na hatua zilizochukuliwa mpaka sasa na ofisi yake katika kupambana na vitendo vya kiharifu kwa ngazi ya kata huku akiahidi kulifanyia kazi wazo la kuhamasisha wananchi juu ya kuwa na vikundi vya ulinzi shiriki katika maeneo yao ili kupambana na kadhia hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...


No comments:
Post a Comment