Search This Blog

Saturday, June 1, 2019

Esperance watwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika


Timu ya Esperance kutoka Tunisia imefanikiwa kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco bao pekee la mshambuliaji Mualgeria Mohamed Youcef Belaili dakika ya 41.

Kwa matokeo hayo, Esperance inayofundishwa na kocha Mtunisia, Moine Chaabani inabeba taji hilo kwa ushindi wa jumla wa 2-1 kufuatia sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa Prince Moulay Abdallah mjini Rabat.

Hilo linakuwa taji la pili mfululizo kwa Esperance na la nne jumla kihistoria, baada ya awali kulitwaa katika miaka 1994, 2011 na 2018.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...