Search This Blog
Wednesday, June 12, 2019
DC Dodoma apiga marufuku mifugo kuingia uwanja wa Ndege
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi amepiga marufuku kwa wananchi kuingiza mifugo, kupita au kufanya shughuli zozote ndani ya uwanja wa ndege kwani ni kosa kisheria.
Ametoa katazo hilo jijini Dodoma wakati wa ziara akiwa ameambatana na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya kutembelea uwanja huo na kuona utendaji kazi ndani ya uwanja wa ndege uliopo mtaa wa Makole Jijini hapa amesema ni marufuku kwa mwananchi yeyote kuingia na kufanya shughuri ndani ya uwanja wa ndege kwamba ni kosa kisheria.
Na kuagiza Wizara ya mifugo kwa kushirikiana na halmashauri ya jiji kuondoa mifugo yote inayozagaa ovyo mjini hasa mbwa, na kwamba ndio inayosababisha kuingia ndani ya uwanja wa ndege kwamba ni hatari kwa wasafiri wanaotumia uwanja huo na kuagiza kila mwananchi kuhakikisha haruhusu mifugo yake kuzagaa mjini.
“Nimetembele uwanja huu mifugo inazagaa ovyo kama unavyoona hapo tumeona mbwa wako ndani ya uzio hii ni hatari kwa wasafiri na ndege inapopaa na kutua, niagize sasa wizara ya mifugo kuhakikisha mnaondoa mifugo yote inayozagaa mjini na wananchi wahakikishe wanawadhibiti wanyama wao wasitembee ovyo,” amesema Katambi.
Aidha amepiga marufuku kwa wananchi kuchoma moto jirani na uwanja huo, akibaini baadhi ya maeneo kuchomwa moto ndani ya uwanja atawawajibisha wale wote ambao wanaishi jirani na eneo ambalo moto huo umetokea, amepiga marufuku kwa waliokuwa wakihujumu miondombinu ya uwanja hasa kwa watengeneza heng’a za nguo kwa kukata senyenge za uzio wa uwanja.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment