Search This Blog

Saturday, June 8, 2019

DC atoa miezi miwili kwa Mkandarasi kukamilisha ujenzi wa stendi


Mkuu wa Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, Festo Kiswaga ametoa muda wa miezi miwili kwa mkandarasi anayejenga stendi mpya ya mkoa kuhakikisha anakamilisha ujenzi huo ndani ya muda huo.

Ujenzi wa stendi hiyo umegharimu Sh. bilioni 7.2 na unatekelezwa na mkandarasi Kings Builders na Construction Co. Ltd kutoka Dar es salaam ambapo umefikia asilimia 68 ya ujenzi wake.

Kiswaga ametoa agizo hilo jana, baada ya kutembelea mradi huo, ambapo alisikitishwa kuona ujenzi umesimama kwa muda wa mwezi mmoja bila ya sababu za msingi.

“Mradi huu ulitakiwa kukamilika Mei, mwaka huu lakini hadi leo bado ujenzi haujakamilika, fedha zipo, mkandarasi umelipwa zaidi ya Sh. bilioni tatu, lakini kazi zimesimama, ndani ya miezi miwili nataka ujenzi ukamilike,” amesema Kiswaga.

Kiswaga pia amemuonya miandarasi huyo endapo hatakamilisha ujenzi huu ndani ya muda huo hatua kali zitachukuliwa ikiwamo kuvunjwa kwa mkataba kwani sababu zilizotolewa hazina msingi wananchi na serikali tunachotaka ni mradi ukamilike.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...