Search This Blog
Thursday, May 23, 2019
Waziri wa Uingereza na mkereketwa wa Brexit ajiuzulu
Waziri anaehusika na masuala ya bunge wa Uingereza Andrea Leadsom, amejiuzulu nafasi hiyo kuhusiana na ubishani juu ya mkakati wa Uingereza kuondoka katika Umoja wa Ulaya.
Katika barua yake aliotuma kwa waziri mkuu May, Leadsom amesema hana tena imani kwamba mkakati wa May utaweza kutekeleza matokeo ya kura ya maoni ya Brexit.
Amekosoa hasa mpango mpya wa kiongozi huyo kuliruhusu bunge kupigia kura pendekezo la kuwa na kura ya pili ya maoni.
Leadsom ambaye ni muungaji mkono wa Brexit, alikuwa anashughulikia uhusiano wa bunge la wawakilishi katika baraza la mawaziri la May, na kujizulu kwake kunazidi kudhoofisha nafasi ya May katika mchakato mzima wa Brexit.
http://bit.ly/2JZwol1
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment