Search This Blog
Thursday, May 23, 2019
Singida United wapishana na mamilioni
Baada ya timu ya Singida United kufungwa mabao 2-0 na Simba juzi Uwanja wa Namfua uongozi wa Singida United umesema kuwa wamepishana na mamilioni ambayo yalitengwa kwa ajili ya ushindi wao.
Ofisa Habari wa Singida United, Cales Katemana ameeleza kuwa waliwaambia wachezaji wao kwamba endapo watashinda kila mmoja angepata kiasi cha shilingi laki mbili na viongozi wa mkoa waliongeza dau kufikia milioni kwa atakayefunga bao.
"Haikuwa bahati yetu na wachezaji wetu walipambana wameshindwa hivyo wamepishana na fedha ambazo zilikuwa zimetengwa kwa ajili yao kwani mbali na milioni sita ambazo zilitengwa na timu viongozi na wadau waliweka mezani milioni moja kwa kila bao.
"Kila kitu kilikuwa wazi maana mchezo wa mpira haufichiki, hivyo hamna namna nyingine wachezaji wamekosa milioni kwa kuwa hakuna aliyefunga, kasi yetu tunailekeza kwenye mchezo wetu wa mwisho dhidi ya Coastal Union utakaochezwa mkoani Tanga," amesema Katemana.
http://bit.ly/2X71xqA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment