Search This Blog

Tuesday, May 28, 2019

Sababu za watu kukunua bidhaa katika biashara yako


Linapokuja swala la kuchagua bidhaa moja dhidi ya nyiingine, watumiaji (iwe wana ufahamu au wasio na ufahamu), kuna vitu huzingatiwa. Katika kuandaa mambo haya, itakuwa sahihi kujenga makundi mawili tofauti.

Kuna sababu zinazosababishwa na bidhaa na zile zisizo sababishwa na bidhaa
Sababu zinahusiana moja kwa moja na bidhaa yenyewe. Kwa mfano, ikiwa umekwenda kununua bidhaa fulani na unapata bidhaa mbili zinazofanana, unaweza kuchagua moja dhidi ya nyingine kwa sababu zote zimetengenezwa katika ufanano sahihi.

Sababu zisizo sababishwa na bidhaa husika. Hizi ni zile sababu zisizo husiana moja kwa moja na bidhaa yenyewe, lakini bado uathiri uamuzi wa mteja katika kufanya manunuzi. Sasa tutazame  mambo matano yasiyo sababishwa na bidhaa ambayo yanajumuisha mtazamo wa biashara, ambayo unahitaji kuyazingatia haya kama unavyofanya kwenye bidhaa zenyewe.

Jina la bidhaa/Huduma
Jina la bidhaa ni kitu kikubwa sana na hatuzungumzi si tu juu ya usawa wa bidhaa bali namna jina lenyewe liinavyoonekana na picha zinazotokeza kwa kuitazama hii huathiri uamuzi wa mnununuzi. Ndiyo maana kuja na majina mazuri ya kampuni ni kazi muhimu sana wakati wa uzinduzi wa jina au bidhaa.

Uwekaji wa Bidhaa/Huduma
Katika mazingira ya kawaida ya uuzaji wa bidhaa, uwekaji au upangaji wa bidhaa ni muhimu sana, ni dhahiri kuona matokeo mazuri zaidi ikiwa bidhaa yako iko kwenye eneo la wazi lenye kuonekana na kila mtu dhidi ya ile bidhaa ambayo iko kando, chini kwenye kona ya nyuma ambako wateja haawezi kuona, kama ni huduma fulani mfano kunyoa nywere au kusuka, weka mahali pa wazi amabako ni rahisi kuonekana. Hii haihusiani na bidhaa yenyewe, lakini inahusiana kabisa na eneo hata kama unaweza kuwa na wateja wako wa kudumu ila ni vyema kuongeza wateja wapya.

Ufungaji 
Wakati wengine wanasema kuwa ufungaji ni jambo linalohusiana na bidhaa, wengi wanaweza kukubaliana nami kuwa ikiwa utaondoa kifungashio na kuiweka ikiwa tupu hapo tutasema kifungashio siyo sehemu ya bidhaa yenyewe, inakupasa kutumia muda mwingi, akili nyingi na jitihada za kukamilisha ufungaji ikiwa unataka kunyakua na kuathiri maamuzi ya kununua. Kifungashio katika bidhaa yeyote huchochea vitu vifuatavyo;

Kuvutia wanunuzi
Uhamasisha manunuzi kuionekana niya kipekee kwa kulinganisha na thamani ya pesa
Inapaswa kuambatana na nafasi au jina la bidhaaa yako na kubaki halisi kwa muda wote.

Sifa
Katika wakati ambao mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vinaleta ufalme, nipale wateja wako wanapoamua kwa vinywa vayo kusifia bidhaa yako, hii itapelekea hata wale ambao bado hawajaijaribu kuweza kuhitaji kuipata hii inakusaidia kukuza na kudumisha sifa nzuri. wateja wako wa sasa wanavyosema kuhusu bidhaa yako watakusaidia kuuza zaidi  au kuondokana na biashara.

Bei
Sababu ya tano isiyo ya bidhaa ambayo wanunuzi wanafikiria sana kabla ya yote ni bei. Changamoto hapa ni kuamua tu jinsi bei inavyoendana na soko la bidhaa zako lilivyo. Katika maeneno mengine bei ni ya kwanza mengine yanakuja namba moja  na katika maeneo mengine ubora wa bidhaa pamoja na soko huzingatiwa kabla ya bei.

Bei 44.2%
Ubora 26.3%
Huduma 13.5%
Muonekano 7.8%
Machaguo 8.3%
Kwa maana hii basi wanunuzi wengi duniani huzingatia swala bei ya bidhaa au huduma.

Sababu za jumla ambazo humpelekea mnunuzi kununua bidhaa au huduma Fulani soma hapa



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...