Search This Blog

Friday, May 24, 2019

RC Aliyetenguliwa na Rais Magufuli Atoa Neno kwa Watanzania



Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Amos Makalla amekabidhi rasmi ofisi kwa Mkuu wa mkoa wa mpya wa Katavi Mh. Juma Zuberi Homela ambaye aliteuliwa na Rais Dkt, John Pombe Magufuli hivi karibuni.


Akizungumza katika makabidhiano hayo amesema amekitumikia Chama cha Mapinduzi (CCM) na Umoja wa vijana (UVCCM) kwa Muda mrefu na vipaji, uzoefu alionao atandelea kuwa Kada mwaminifu wa mstari wa Mbele wa Chama cha Mapinduzi

Amos Makalla amemshukuru Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kumuamini na kumteua katika  nafasi ya Ukuu wa Mkoa kwa miaka minne iliyopita akiitumikia mikoa ya Kilimanjaro, Mbeya na Katavi katika uongozi Serikali ya  Awamu ya Nne na ya Tano

Amesema mwaka 2015 Alipokosa Ubunge ilitosha yeye kubaki mwananchi na mwana (CCM) tu huko Mvomero lakini Rais wa awamu ya nne  Mhe Jakaya Kikwete alimteua kuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro na pia Rais Dkt. John Pombe Magufuli alimteua kuwa mkuu wa mkoa wa Mbeya na baadaye Katavi.

Amewashukuru wananchi na viongozi wa ngazi zote dini na serikali kwa kumpa ushirikiano katika Kipindi cha miezi 10 alipokuwa mkuu wa mkoa wa Katavi na Amewaomba wananchi na viongozi wampe ushirikiano wa kutosha mkuu wa mkoa Mpya Juma Homela.

http://bit.ly/2JD8z3g

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...