Search This Blog
Saturday, May 25, 2019
Rais wa China atuma salamu za pongezi kwa Waziri Mkuu wa India
Rais wa China Xi Jinping ametuma salamu za pongezi kwa Waziri mkuu wa India Narendra Modi baada ya chama chake cha Bharatiya Janata BJP kushinda kwenye uchaguzi.
Programu ya simu ya mkononi ya Tume ya Uchaguzi ya India ECI imetangaza ushindi wa chama cha BJP katika uchaguzi mkuu wa 17 uliomalizika hivi karibuni.
Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na ECI, chama hicho kimepata kura 272, idadi ambayo imefikia kigezo cha nusu ya kura zote cha kuanzisha serikali. Kura za chama hicho zinaonekana kuendelea kuongezeka, wakati wagombea wa chama hicho wakiongoza katika majimbo 31 zaidi ya bunge. Kura bado zinaendelea kuhesabiwa.
Katika ujumbe huo,Xi alisema kuwa China na India ni majirani muhimu kwa kila mmoja na ni nchi mbili zinazoendelea zaidi kiuchumi duniani.
Uendelezaji wa mahusiano ya China na India umepata nguvu kubwa katika miaka ya hivi karibuni kutokana na jitihada za pamoja za pande hizo mbili, alisema rais wa China, akiongeza kuwa nchi hizo mbili zinaendeleza uwiano mzuri na ushirikiano juu ya masuala makubwa kama vile kukuza utandawazi wa uchumi na kuimarisha ushirikiano wao.
http://bit.ly/2wiVVh1
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment