Search This Blog

Sunday, May 26, 2019

Rais Magufuli Ageuka 'Mpigapicha' Rais Ramaphosa

RAIS John Magufuli leo Jumamosi Mei 25, 2019, amekuwa kivutio nchini Afrika Kusini baada ya kugeuki fani ya kupiga picha katika hafla ya kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo leo, Cyril Ramaphosa.

Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na viongozi wa nchini mbalimbali, akiwemo Rais Magufuli na Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kiwete kuliibuka matukio mengi ya kufurahisha.

Moja kati ya matukio hayo ni kitendo cha Rais Magufuli kutumia simu ya mkononi kuwapiga picha Rais Ramaphosa na Kikwete.

Tukio hilo limevuta hisia za watu wengi katika mitandao ya kijamii na kushangazwa na Rais Magufuli jinsi alivyoshikilia vyema simu hiyo na kuwapiga picha wawili hao.

Viongozi hao walionekana kufurahia tukio hilo wakiwemo baadhi ya marais wa mataifa mengine waliokuwa pembeni yao.




http://bit.ly/2wiQJtD

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...