Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam mnamo tarehe 25/05/ 2019 majira ya saa nane usiku huko maeneo ya Kigogo Fresh Mtaa wa Seremala lilifanikiwa kuwaua majambazi watatu akiwemo mwanamke mmoja na kisha kukamata bastola mbili aina ya Browning zilizofutwa namba na risasi tatu .
Awali jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam lilipata taarifa kutoka kwa msiri kuwa kuna kikundi cha majambazi wapatao watano wamepanga kuvamia nyumba ya Bwana ALLY DASTAN (66), Mkazi wa Kigogo Fresh ambaye mke wake aitwaye MOSHI SAID(56) ni Mwenyekiti na ni mtunza hazina wa Kikundi cha Umoja Group.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam kupitia kikosi kazi Maalum cha kupambana na ujambazi kiliweka mtego katika nyumba ya Bwana ALLY na ilipofika majira ya saa nane usiku majambazi hao wapatao watano walivamia nyumba hiyo na baada ya kugundua kuwa kuna mtego wa polisi walianza kurusha risasi na ndipo askari wakajibu mapigo na kufanikiwa kuwajerui majambazi watatu akiwemo mwanamke mmoja na majambazi wawili walikimbia. Majambazi hao walifariki dunia wakiwa njiani wakipelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linaendelea kuwasaka majambazi wawili waliokimbia.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment