Search This Blog
Sunday, May 26, 2019
Nimeamua Kutembea Kimapenzi na Binti wa Kazi, Sina Jinsi...
Nina mke na watoto 3 wote tunafanya kazi. Tulipozaa mtoto wa pili wife alianza kupunguza umuhimu wa tendo la ndoa sijua ni kwa kuzoea au kuchoka.
Tumewekana vikao vyetu binafsi ili kila mmoja abainishe ni vichocheo gani vinakosekana ili tuviongeze kuboresha mchezo. Wote siyo walevi na tuko karibu kifamilia. Ukifuatilia labda mkeo ana mtu hupewi taarifa zozote mbaya. Sasa tatizo ni kitu gani hatujui. Ukimwuliza naye anakwambia mume wangu nivumilie nitajitahidi ila baada ya mwezi anarudi kule kule. Usipochombeza anaweza kupitiliza hata mwezi bila kukumbushia huku tukiendelea kuheshimiana kwa sana na peace na upendo ukitawala katika nyumba.
Hali hii imenisumbua kwa muda karibu 7 years na ili kuepuka kugombana na kuepuka kwenda nje kupata UKIMWI basi nikaamua nimweleze binti ambaye anatusaidia kazi home na akaonyesha kunisikitikia kwani mi si mtu wa baa useme ningetafuta huko na pia naogopa UKIMWI. Binti akasema anaweza ku handle hiyo situation kwa masharti kwamba ataendelea kuniheshimu mimi pamoja na wife ili chochote kisishtukiwe.
Kwa mtazamo wangu hata kama mtaniona blind ni kwamba huyu binti anatumika ku rescue hii situation la sivyo ningekwenda huko na huko kutafuta viruka njia ambao wangeniweka mahali pabaya zaidi. Tumeanza mahusiano vizuri na tunaendelea kiasi kwamba hata wife asipokuwa tayari mwezi mzima sipati shida na hii imenisaidia kuepuka ugomvi uliokuwa unatokana na tendo la ndoa kutokuwa zuri. Cha ajabu hata kama mchezo tusipofanya na wife mwezi anaona mambo iko sawa maisha yanaendelea ni kucheka na kufurahi bila kujiuliza huyu mume anaishije?
Je wadau katika situation kama hiyo ambayo mke ana behave namna hii kwa ninachokifanya nimekosea au niko sawa. Kama unafikiri nimekosea nipe ushauri kuhusu njia mbadala na jiweke kwenye position yangu.
http://bit.ly/2QruYRt
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment