Search This Blog

Saturday, May 25, 2019

Nilikuwa Napenda Kushindanishwa na Ruby, Mama Yangu Anampenda - Nandy



Msanii wa Muziki Bongo, Nandy amesema kuwa mama yake anampenda sana Ruby na anapenda muziki wake.

Kauli hiyo imekuja baada ya wasanii hao kushindanishwa mara nyingi mtandaoni, jambo ambalo Nandy amesema sio kitu kibaya kushindanishwa nae kwasasa msanii huyo ana uwezo.

"Mama anampenda sana Ruby anapenda muziki wake na tunasikiliza sana nyimbo zake,  mimi kufanya kazi na Ruby bado hatujawaza japokuwa ni msanii mzuri na itakapofikia hatua ya kufanya kazi tutafanya tu," alisema Nandy.
"Hatujawahi kuwa karibu na namba yake sina, nilikuwa napenda kushindanishwa nae , ukishindanishwa na kitu kibaya ndio utachukia, ukishindanishwa na kitu kizuri inaonyesha na mimi uwezo wangu ni mzuri nilikuwa napenda na naona sawa tu."


http://bit.ly/2HB3xSv

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...