Search This Blog

Saturday, May 25, 2019

Migogoro ya ardhi Tarime yashika kasi

Na.Timothy Itembe Mara

Matukio ya migogoro ya Ardhi wilayani Tarime mkoani Mara imeonekana kushika kasi kuliko matrukio mengine katika jamii.

Mkuu wa wilaya Tarime mkoani Mara,Charles Kabeho alisema jana katika kikao cha Mafunzo ya Viongozi wa Umma na watumishi wa Umma kilichofanyika katika ukumbi wa Shule ya sekondari ya Tarime na kuwashirikisha madiwani pamoja na watumishi wa halmashauri za Tarime vijijini na Tarime Mjini.

Kabeho alisema kuwa katika Ofisi yake anapokea malalamiko ya Migogoro ya Ardhi kwa wingi kuliko malalamiko ya matukio mengine klatika wilaya hiyo.

"Ndugu zangu Watumishi pamoja na Madiwani mliopo hapa tujaribu kumsaidia Rais awamu ya Tano,John Pombe Magufuli katika kutatua migogoro inayowakumba wanancxhi badala ya kuendelea kukaa na kufumbia macho kero zinazowakabili wananchi hata hivyo katika wilaya Tarime kiuna migogoro mingi ya Ardhi ninayopokea katika Ofisi yangu kwahali hiyo tusaidie Raisi wetu kazi"alisema Kebeho.

Kwa upande wake, Godson Peter Kweka katibu msaidizi wa sekereterieti ya maadili ya viongozi wa Umma kanda ya Ziwa ambaye pia alikuwa mwezeshaji katika semina hiyo alisema kuwa sekereterieti ya maadili ya viongozi wa umma ilianzishwa ili kusimamia utekelezaji wa sheria ya maadili ya viongozi umma namba 13 ya mwaka 1995 kama ilivyorekebishwa na sheria namba 5 ya mwaka 2001 pamoja na sheria namba 4 ya mwaka 2016.

Kiongozi wa umma anatakiwa kufanya kazi kwa uaminifu, uadilifu, upole na kwa njia inayokuza imani ya wananchi kuhusu uwadilifu wa viongozi wa umma katika utekelezaji wa shuguli za umma.

Pia katibu huyo aliongeza kuwa semina hiyo imelenga majukumu ya sekreterieti ya maadili ya viongozi wa umma,mamlaka ya sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma na misingi ya maadili ya viongozi wa umma na watumishi wa umma.

Naye mkurugenzi wa halmashauri ya Tarime vijijini,Apoll Tindwa alipongeza Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma kanda ya ziwa kuleta semina hiyo kwa wakati ambapo alisema kuwa hapo nyuma viongozi walikuwa na mgongano wa kimasilahi.

Tulikuwa na mpasuko ndani ya viongozi huku baadhi ya viongozi wakiwa wanvujisha siri za Serikali jambo ambalo nikinyume lakini kwasasa baada ya kupata semina hii tunategemea viongozi kila moja ataenda kufanya yaliyohaki lengo likiwa ni kutumikia Jamii.

Mwenyekiti wa halmashauri ya Tarime Mjini,Khamis Nyanswi alisema kuwa semina hiyo imekuja nje ya wakati ambapo viongozi wakuchaguliwa kama vile madiwani wanenda kumaliza mda wao wa kuchaguliwa.

http://bit.ly/2X9kTv2

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...