Search This Blog

Tuesday, May 28, 2019

Harry Kane kuivaa Liverpool


Harry Kane anatarajiwa kukwea pipa na kikosi chake cha Tottenham siku ya Jumatano kuifuata Liverpool kwa ajili ya mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Mshambuliaji huyo amekuwa kwenye maandalizi ya kikosi kinachojiandaa kuivaa Liverpool kwenye fainali itakayopigwa siku ya Jumamosi alikuwa nje kutokana na kusumbuliw na majeruhi.

Maendeleo ya mshambuliaji huyo yamekuwa yakiridhisha hali inayotoa nafasi kubwa kwake kuweza kuanza kwenye kikosi kitakachoshuka uwanja wa Wanda Metropolitano.

Meneja wa Totthenham, Mauricio Pochettino anahitaji kumpa nafasi mshambuliaji huyo ili kujua kiasi gani amekuwa imara baada ya kupata majeruhi.

"Kumuanzisha yeye ndani ya kikosi ndiyo kitu ambacho ninakifikiria itakuwa ni maamuzi yangu mwenyewe kumuazisha ama kutomuanzisha kwenye mchezo huo ama michezo mingine, itategemea na namna atakayofanya kama tukishinda itakuwa furaha tukipoteza ni mbaya kwetu," amesema.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...