Search This Blog
Wednesday, May 29, 2019
DC Kongwa atinga mnadani kugawa vitambulisho, wajasiriamali wampongeza Rais Magufuli
Na. Enock Magali,Kongwa Dodoma
Mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge May 27 kufanya ziara wilayani Kongwa kwa ajili ya kuhamasisha suala la vitambulisho vya wajasiriamali,Mkuu wa wilaya hiyo, Deo Ndejembi leo ametembelea katika mnada wa Mkutani na kufanikiwa kuuza vitambulisho 54.
Akiwa anaendesha zoezi hilo baadhi ya wajasiriamali katika mnada huo wamempongeza Mheshimiwa Rais Dkt.John Pombe Magufuli kwa uamuzi wake wa kuwapatia vitambulisho hivyo vinavyowawezesha kufanya biashara kwa uhuru popote watakapokuwa ndani ya nchi.
"Kwa kweli Mkuu wa Wilaya tuseme tu ya kwamba,tunamshukuru sana Rais wetu Magufuli kwani mwanzo tulikua tunalipia tozo na ushuru zaidi ya laki moja kwa mwaka,lakini baada ya kukata hivi vitambulisho saivi hatulipii chohote,sisi wajasiriamali kwa Kongwa tumefurahi sana"Alisema mmoja wa wafanyabiashara.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya hiyo amewatoa hofu wajasiriamali hao na kusema kuwa kwa yoyote aliekata kitambulisho hatosumbuliwa kwa tozo bali wafanye kazi zao kwa uhuru kwani Mheshimiwa Rais amewapendelea kwa kiasi kikubwa.
"Mmefanya jambo jema kukata vitambulisho,mmeunga juhudi za Rais weu katika kuiletea nchi maendeleo,fanyeni biashara kwa uhuru kwani hakuna mtu atakaye wasumbua tena kwenye masuala ya tozo na ushuru,lakini pia waambieni na wenzenu wakate vitambulisho hivi kwani bila kufanya hivyo hawatoruhusiwa kufanya biashara,lazima tuelewane kwa hilo"Alisisitiza.
Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa Wilaya amesema kuwa jumla wamepewa vitambulisho 11250 ambapo hadi sasa wamebakiza vitambulisho 3707 pekee.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...
No comments:
Post a Comment