Mkazi wa Mtaa wa Tagota Halmashauri ya mji Tarime mkoani Mara, Muniko Kinyunyi (30) amekufa kwa kuchomwa na kisu shingoni baada ya kutokea ugomvi na mwenzake ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja.
Wawili hao wanadaiwa kuwa walikuwa wakigombea mwanamke katika sherehe iliyofanyika nyumbani kwa aliyekuwa mgombea ubunge mwaka 2015 Jimbo la Tarime Mjini, Michael Kembaki.
Kwa mujibu wa diwani wa Kenyamanyori, Ganga Mgendi tukio hilo la kusikitisha lilitokea usiku wa kuamkia jana nyumbani kwa Kembaki Tarime mjini.
Kembaki katika uchaguzi huo wa mwaka 2015 aliwania nafasi hiyo ya ubunge Tarime Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuangushwa na mbunge wa sasa, Esther Matiko (Chadema).
Mgendi alisema tukio hilo lilitokea wakati wa sherehe iliyofanyika nyumbani kwa mwanasiasa huyo aliyetembelewa na dada yake aliyekwenda na kikundi cha watu kuwasalimia mama na ndugu zake.
Alisema katika shamrashamra hizo ndipo kulipoibuka ugomvi kati ya Mniko na mtu ambaye hakufahamika mara moja jina lake wakigombea mwanamke hali iliyosababisha mtu huyo kumchoma Mniko kisu shingoni karibu na kifuani na kisha kutoroka wakati watu wakihangaika kumkimbiza katika Hospitali ya Wilaya Tarime ambapo alifariki kabla ya kupatiwa matibabu kutokana na kutokwa damu nyingi.
Kamanda wa Polisi Tarime Rorya, Henry Mwaibambe alithibitisha kutokea kwa tukio hilo la mauaji na kueleza kuwa Jeshi la Polisi linamsaka mtuhumiwa na kuwaomba raia wema kutoa ushirikiano ili kuweza kumkamta mtuhumiwa huyo aliyetoroka.
http://bit.ly/2WcfZBe
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment