Search This Blog

Monday, May 27, 2019

Aliyepotea mazingira ya kutatanisha akutwa kajinyonga juu ya mti



Na James Timber, Mwanza

Mkazi wa kijiji cha Nyakahako Kata Chifunfu Wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza aliyekuwa amepotea katika mazingira ya kutatanisha amepatikana akiwa amejinyonga juu ya mti.

Afisa Mtendaji  Kata ya Chifunfu Kisaba Masangwa alimutaja aliyekumbwa na tukio hilo kuwa Tumaini Faustine [35] mkazi wa kijiji cha Nyakahako wilayani humo.

‘’Kablaya kugundulika akiwa amejinyonga taarifa za kupotea kwake zililipotiwa ofisini kwangu na jitihada za kumutafuta zikiwa zinaendelea aligundulika akiwa amejinyonga  mei 25 majira ya saa 2.30 za usiku,’’alisema  Masangwa.

Kaimu mganga mkuu kituo cha afya ya Ngomamtimba kilichoko kata ya Chifunfu John Ishengoma alisema baada ya mwili huo kufanyiwa uchunguzi ulikutwa na majeraha shingoni, kichwani kama kapigwa na kitu chenye nchi kali pamoja na kutokwa damu masikioni na kuzua utata juu ya kujinyonga kwake.

Baba wa kijana huyo ambaye ni marehemu Mzee Imani Faustine alisema kijana wake alitoweka siku tatu zilizopita nyumbani kwake katika mazingira ya kutatanisha na hapakuwa na ugomvi wa aina yoyote na kusikitishwa na tukio la mwanaye kujingonga.

Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Emmanuel Kipole alisema amekwisha pata taarifa juu ya tukio hilo na kusema kuwa mtu huyo kwa mjibu wa Madakitari hakujinyonga bali alinyongwa na mwili wake kutundikikwa juu ya mti kwa kuwa ulikutwa na majeraha shingoni na kichwani kuwa alipigwa na kitu chenye nchi kali na uchunguzi bado unaendelea kuwatafuta waliofanya kitendo hicho.

http://bit.ly/2HXacW8

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...