Search This Blog

Monday, October 11, 2021

Waziri wa mambo ya kigeni ya Austria kuwa kansela mpya


Waziri wa mambo ya kigeni wa Austria Alexander Schallenberg anatarajiwa kuchukua nafasi ya ukansela baada ya kansela wa sasa Sebastian Kurz kujiuzulu. Kurz aliyeongoza serikali kwa awamu mbili katika kipindi cha miaka minne amempendekeza Schallenberg kuchukua nafasi hiyo ya juu, baada ya kujiuzulu siku ya Jumamosi kufuatia madai ya ufisadi yanayomkabili. Amesema amechukua hatua hiyo ili kuepusha ghasia. Schallenberg ambaye amekuwa waziri wa mambo ya kigeni tangu mwaka 2019, amenukuliwa akisema halitakuwa jukumu jepesi kwake. Waziri huyo pia amekutana na rais Alexander Van der Bellen na anatarajiwa kuapishwa siku chache zijazo.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...