Search This Blog

Monday, October 4, 2021

Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed kutangaza baraza jipya la mawaziri


Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed anatarajiwa kuapishwa na kuunda baraza jipya la mawaziri Jumatatu, kufuatia uchaguzi wenye utata wa mwezi Juni mwaka jana uliompatia ushindi wa kishindo chama chake.

Ushindi wa chama chake, uligubikwa na vita vilivyosababisha mauaji katika jimbo la kaskazini mwa nchi hiyo la Tigray.

Ushindi huo unamaanisha kuwa Bw Abiy atabakia mamlakani kwa miaka mitano zaidi ijayo.

Bw Abiy aliingia mamlakani kwa mara ya kwanza katika mwaka 2018, kufuatia miaka ya maandamano dhidi ya serikali.

Wakati huo alikuwa mtu ambaye hakuwa maarufu kisiasa ambaye ghafla aliikonga mioyo ya mamilioni kutokana na hatua zake za mageuzi. Kuongezeka kwa makabiliano ya mara baada ya kuingia katika mamlaka lilikuwa tatizo kuu kwake.

Lakini changamoto kubwa ilikuja yapata mwaka mmoja uliopita wakati vita vilipoibuka katika Tigray. Maelfu wanaaminiwa kuuawa na pande zote husika na mzozo huo.

Abiy ambaye wakati mmoja alikuwa kipenzi cha jamii ya kimataifa na kupewa tuzo ya amani ya Nobel, utawala wake kwa sasa unashutumiwa kuzuwia misaada kwa Tigray.

Uchaguzi wa mwezi Juni ulitawaliwa na utata, huku baadhi ya makundi makuu ya uoinzani yakiususia. Katika serikali mpya, Bw Abiy atakabiliwa na matatizo ya zamani, huku kupata suluhu ya vita vya Tigray likiwa tatizo kuu linalohitaji kupatiwa suluhu ya haraka.


 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...