Search This Blog
Tuesday, September 14, 2021
Mkuu wa Wilaya tunabebwa kama mizoga hatuna waganga wa kutosha
Na Maridhia Ngemela. Mwanza.
Wananchi wa kata ya Sangabuye wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza wamemuomba mkuu wa wilaya hiyo kuwapatia wahudumu wa afya wa kutosha kutokana na adha wanazopata katika sekta ya afya.
Nestori mashibeli ni miongoni mwa wananchi waliopata nafasi ya kuelezea changamoto zinazowakabili na amezungumzia juu ya sekta ya afya na elimu ameiomba serikali kuongeza waganga wafawidhi wa kituo cha afya cha sangabuye kutokana na wingi wa wananchi wanaopatiwa huduma hiyo na uhaba wa vyumba vya madarasa,uhaba wa walimu imekuwa ni changamoto kubwa kwa wanasangabuye.
Amesema"kituo cha afya cha sangabuye kina mganga mfawidhi mmoja,hicho kituo kinahudumia kalibia kata tatu Lutale, sangabuye na kayenze kama itawezekana kituo hicho kiongezewe waganga hata wawe wawili ikitokea mgonjwa yuko hoi atafia pale kutokana na ukosefu wa waganga, hakuna mochwari tunabembwa kama mizoga alafu mkuu wa wilaya sangabuye tuna uhaba wa walimu na madarasa lakini pia nyumba za watumishi hakuna tunataka utwambie leo hizi changamoto zitaisha lini?amesema Mashibeli"
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masala alipokuwa akijibu kero za wananchi amekerwa na baadhi ya watendaji wa Serikali wasiokuwa waaminifu katika kufanya maendeleo na kula fedha za Serikali zinazotolewa kwa lengo la maendeleo watendaji tufanye kazii kama timu kwa kufuata miongozo.
Masala amesema"kuna fedha zilipelekwa shule ya sangabuye zimepigwa na sijajua hatua zipi zilichukuliwa isionekane serikalinzima tunashindwa kusimamia fedha zilizoletwa kwaajili ya kujengewa bwalo na mabweni tunataka fedha zetu awe amehamishwa au mshahara ukatwe naomba nipate hatua zilizochukuliwa kwa huyu mwalimu aliyefuja fedha za Serikali ,hizi fedha zingefanya Jambo kingine,msianze ujenzi wote mpaka tumalize hili Jambo Mkurugenzi naomba utusaidie hizi fedha zilikuwa za kujenga madarasa sijaja hapa kupigiwa makofi na wananchi.
Amesema kuwa upande wa barabara wananchi waweze kuchangia mafuta kwa kushirikiana na viongozi wa mitaa waite magari ili waweze kuchonga barabara ambazo zinawezekana huku wakisubiria bajeti za kubwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...

No comments:
Post a Comment