Search This Blog

Monday, September 6, 2021

Hassn Kessy sini mkataba wa mwaka mmoja KMC


UONGOZI wa KMC umetangaza rasmi kumpa dili jipya nyota aliyekuwa anakipiga ndani ya Mtibwa Sugar ya Morogoro.

Kupitia ukurasa wao wa Instagram leo Septemba 5 wameandika namna hii:" Tunathibitisha usajili wa Hassan Khamis Ramadhani “Kessy” kutoka Klabu ya Mtibwa Sugar kwa Mkataba wa mwaka mmoja. Karibu sana Kinondoni Kessy.

Kessy ambaye aliwahi kucheza ndani ya Klabu ya Yanga na Simba ndani ya ardhi ya Tanzania alipata nafasi pia kukipiga ndani ya Nkana FC ya Zambia.

Alirejea Bongo msimu uliopita na kujiunga na Mtibwa Sugar iliyonusurika kushuka daraja kwa kucheza play offs.

Kwa sasa atakuwa ndani ya KMC ambayo imeweka kambi Morogoro kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2021/22.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...