Na Timothy Itembe Mara.
Taasisi isiyo ya kiserikali VISO kwa kushirikiana na TWCC na LEAT wamekuja na mpango mkakati wa suluhisho la kuelimisha jamii juu ya madhara yatakayo wapata watoto chini ya umriwa miaka 18 kuajiriwa migodini.
Akizungumza na waandishi wa habari ukumbi wa hoteli ya CMG iliyopo mjini Tarime mkoani Mara,Clay Mwaifwani kutoka taasisi ya LEAT ambaye ni Afisa mradi alisema kuwa kuajiriwa watoto chini ya umri wa miaka 18 migodini ni ukiukwaji wa sheria na katiba ya Jamhuri ya Tanzania ambapo kufanya hivyo niukikwajiwa sheria na kuwanyima watoto haki zao za msingi.
"Tumekuja na mradi,jitihada za pamoja za ufikiwaji WA haki kwenye sekta ya uzinduaji (CLART) mradi huo unalengo la kuzijengea Taasisi mbalimbali uwezo ili wafanye kazi na kuwafikia Wananchi katika sekta ya madini,mafuta na Gesi na kunufika na rasilimali zilizopo"alisema Mwaifwani.
Rugina aliongeza kusema kuwa mradi wetu unawajengea uwezo taasisi hizo ili kujua mambo mhimu ya madini mafuta na Gesi na changamoto zinazowakabili wakazi wa mazingira yanayozunguka mgodi pamoja na kujua haki za kimsingi na kunufaika na rasilimali zilizopo.
Alitolea mfano wa sheria ya Ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004 kifungu cha 5 ambayo inazuia kabisa mtoto chini ya umriwa miaka 18 kuajiriwa na kutumikishwa na kuwa mazingira hayo niukiukwaji wa katiba ya Jamhuri ya muungano ya Tanzania.
Afisa huyo alitaja sheria nyingine ambayo wanaende kuwaelimsha taasisi na kuwaelimisha wananchi ni pamoja na sheria ya usimamizi wa rasilimali Maji ya 2009 kifungu cha 64 inasema ili utiririshe maji lazima uwe na kibali cha mamlaka ya Bonde.
Naye mshauri wa sera na utawala Bora,Joram Michael Rugina alisema kuwa madhila yanayotokana na uwepo wa shuguli za madini yanawaadhiri wakazi wa naeneo yanayochimbwa.
Lengo letu nikuzijengea taasisi mkakati,mipango,sera sheria za kimataifa zenye lengo la kukabiliana na hizo adhari na changamoto ili kuchukua hatua aliongeza kusema Rugina.
Afisa aliongeza kuwa mradi huu umelenga Wanawake,Vijana na Watu wenye ulemavu namna ya kunufaika na rasilimali zilizopo kama vile za wawekezaji pamoja na serikali kama hawanufaiki wahoji.

No comments:
Post a Comment