Search This Blog

Tuesday, August 10, 2021

Ujerumani yapinga miito ya kuwarudisha tena wanajeshi nchini Afghanistan

 


Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Annegret Kramp Karrenbauer amepinga miito juu ya kuwarejesha wanajeshi wa Ujerumani nchini Afghanistan baada ya wataliban kuuteka mji wa Kunduz uliokuwa makao makuu ya wanajeshi hao kwa muda wa miaka 10. 


Waziri Kramp Karrenbauer amesema kuwashinda wataliban kutahitaji muda mrefu na mapambano magumu. Baadhi ya watu ndani ya chama chake cha CDU wanataka wanajeshi wa Ujerumani washiriki katika kuwazuia wapiganaji wa Taliban. 


Waziri huyo ameulaumu utawala wa Trump kwa kuihujumu operesheni ya Afghanistan. Ujerumani ilikuwa inashika nafasi ya pili kwa idadi ya askari kutoka nje, baada ya Marekani. Askari wengi wa Ujerumani waliuawa katika mapigano kwenye mji wa Kunduz, kuliko kwenye sehemu nyingine yoyote, tangu kumalizika vita vikuu vya pili. 


Wataliban wameshaitia mikononi miji mikuu kadhaa ya majimbo ikiwa pamoja na huo wa Kunduz na wanasonga mbele tangu kuanza kuondoka kwa majeshi ya kimataifa kutoka Afghanistan.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...